
Takribani karne moja sasa binadamu wamekuwa ‘wakiitembelea’ dunia kupitia simu za mkononi iwe kwa kupigiana au kutumiana ujumbe mfupi wa maandishi au kuwasiliana katika mitandao ya kijamii.
Kwa wafuatiliaji wa masuala ya teknolojia ‘selfie stick’ sio msamiati mgeni masikioni mwao, lakini kwa faida ya wengine hiki ni kifaa ambacho hutumika kushikilia simu au kamera ndogo wakati wa kujipiga picha kama kinavyoonekana pichani.
OK! Jiandae kwa simu ya mkononi ambaye inaweza kukunjwa na kukunjuliwa kadri upendavyo na kuitupia ndani ya waleti yake yenye ukubwa wowote. Baada ya kutengeneza kila aina ya 'gadget', Samsung inajiandaa kutengeneza simu mpya ambazo zinakunjika; bila shaka hizi zitakuwa hazivunjiki kwasababu lazima zitakuwa za mpira.