EDUCATION HUB::Find education news, events, schools and college in East Africa

Donate Educations

Natafutashule.com: Changia kusaidia watu wenye shida ya elimu

Ni mtandao unashudhulika na masuala ya elimu kwa ujumla,  wadau wake wakubwa ni wazazi, walimu, wamiliki wa shule, wanafunzi na wafanyabiashara.Tunajua elimu ni jambo la muhimu kwa kila mtu ila kutokana na uwezo wa kifedha wazazi na wanafunzi wengi wameshindwa kufikia ndoto zao kielimu..

 Watu binafsi, taasisi, mashirika mbalimbali yamekuwa yakisaidia kuwawezesha baadhi ya wanafunzi na wazazi wakamilishe ndoto zao kielimu kwa kuwalipia ada na gharama mbalimbali za elimu.

Kwa sababu wafadhli wengi wanashindwa kuwafikia wanafunzi, walimu na wazazi wenye matatizo ya kielimu mtandao wa natafutashule umeliona hili hivyo umeamua mbali na shughuli zake zingine kuwa kiunganishi kati watu wenye shida kielimu na wafadhiri.

Katika database yetu hivi sasa wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi wameshindwa kwenda shule ni zaidi ya 4,000, wazadi walioshindwa kupeleka watoto wao shule ni zaidi ya 6,000, walimu wanaotafuta ajira zadi 6,000 na shule zinazotafuta walimu ni zaidi2,000.

Tunapenda kuchukua fursa hii kuwaombea msaada wanafunzi na wazazi walio katika matatizo ya kiuchumi kwa wafadhili mbalimbali duniani kote waweze kuwasaidia ili watimize ndoto zao.

Kwa upande wa walimu tunapenda kuziomba shule zenye upungufu wa walimu kuingia kwenye database yetu na kutafuta walimu wanaowahitaji na kuwaajili. Kwa wafadhili ambao wamegushwa kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo ya kielimu watume michango yao kwenye account hii Standard Chatered Bank, NIC Brach, A/C 0100333001000, swift SCBLTZTX, Dar es Salaam, Tanzania, wanafunzi na wazazi wote watakaopatiwa msaada na wafadhili taarifa zao zitatolewa katika tovuti hii.

Lengo na mipango yetu kuwa taasisi kubwa ya kutoa misaada mbalimbali ya kielimu kwa wanafunzi, wazazi, walimu na shule.

 

You are here: Home Donate Education